Mkuu wa Wilaya ameagiza kuanzia tarehe 27/06/2019 mchimbaji yoyote ambaye atakuwa hana kitambulisho hatoruhusiwa kwenda mgodini kufanya shughuli za uchimbaji.
Pia amepiga marufuku wazururaji wanaoenda Namungo wakiwa hawana shughuli yoyote na hawana vitambulisho cha kuwatambua wanafanya shughuli gani hapo mgodini.
Amesema hayo tarehe 26/06/2019 wakati wa kikao chake na wachimbaji katika eneo la mgodi katika kitongoji cha Namungo kilichopo Kata ya Mbekenyera
Nilazima kila mchimbaji mdogo kuwa na kitambulisho hiki unaitaji kutambulika na serikali kwa shughuli unayofanya nunua kitambulisho hiko.
"Fuateni sheria unajijua huna kitambulisho unafahamu vinapopatikana nunua chako mapema kuanzia kesho nikikukamata huna kitambulisho na unazunguka zunguka tu huku nitakushughulikia" amesema Mgandilwa
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ameuza vitambulisho 243 kwa wachimbaji wadogowadogo baada tu ya mkutano wa kumalizika kama ambavyo alikubaliana nao mkutano uliopita kilichofanyika tarehe 10/06/2019.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa