Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hashim Mgandilwa amewataka watendaji wote wa Kata na Vijiji waliopo Wilayani hapa kutatua kero za wananchi katika maeneo yao kabla wananchi awajaleta matatizo yao katika ofisi yake au Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwani wao ndio wakurugenzi katika maeneo yao.
Mhe. Mgandilwa amesema hayo alipokuwa kwenye kikao kazi alichokiitisha tarehe 22/12/2018 katika ukumbi wa CCM Ruangwa Mjini kwa ajili ya kutoa maelekezo mbalimbali kwa Watumishi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa.
Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka watendaji hao kujipangia ratiba na siku maalumu ya kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
" Najua kuna baadhi ya watendaji hamkai katika maeneo yenu ya kazi, pangeni ratiba muiweke ofisini na muache namba za simu ili usipokuwepo mwananchi aweze kukutafuta kwa njia ya simu"
"Inashangaza unaenda kwenye vijiji unakuta miradi ya maendeleo ila mtendaji wake ajui suala lolote la huo mradi, ni wajibu wenu kujua kila mradi unaoingia katika maeneo yenu" alisema
Wakati huo huo Mhe. Mgandilwa amewataka watendaji wenye namba za simu za viongozi kutumia vizuri namba hizo na kuacha kupiga simu kwa viongozi bila utaratibu.
Amesema anajua kuna watendaji wananamba ya simu ya Waziri Mkuu niwatake muache mara moja tabia ya kumtafuta Mhe, Waziri kwani kuna ofisi unayoweza kupeleka jambo lako hapa hapa Ruangwa na likatatuliwa.
"Ukija ofisini kwangu utaona kuna ofisi ya mbunge na kuna katibu wa Mbunge na katibu wa Waziri Mkuu jimboni acheni kupiga piga simu zisizo na utaratibu huo siyo utaratibu " amesema Mgandilwa
Mhe. Mgandilwa ameitaka ofisi ya Utawala ya Wilaya kufuatilia vikao vya mapato na matumizi katika vijiji kama vinafanyika katika maeneo yao kwani ni wajibu wa wananchi kusomewa mapato na matumizi kila baada ya miez mitatu hata kama hakuna makusanyo ni lazima kikao kifanyike.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ngd. Andrea Chezue ametoa pongezi kwa watendaji kata na vijiji kwa kutimiza majukumu yao kama inavyotakiwa.
Ngd. Chezue amewataka waendele kusimamia suala la ufaulu katika maeneo yao kama walivyofanya katika shule za msingi hadi Kupelekea Wilaya ya Ruangwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya 84 kitaifa kati ya halmashauri 185.
Vile Vilevile amewataka watendaji hao kutatua changamoto za mipaka katika maeneo yao kabla ya kufika kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
MWISHO.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa