Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, ametoa rai kwa walimu wa michezo na wadau wa michezo wilayani Ruangwa kuanzisha shule za michezo, maarufu kama Football Academy, kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20, hatua hiyo inalenga kuongeza tija na kuimarisha sekta ya michezo wilayani Ruangwa.
Akizungumza leo, Desemba 20, 2024, wakati wa kufunga Mafunzo ya Michezo kwa Jamii katika viwanja vya Shule ya Awali na Msingi Wonder Kids, Mhe. Ngoma amesema hatua hiyo itawapa vijana fursa za kujiendeleza katika sekta ya michezo. Mafunzo hayo, yaliyoanza rasmi Disemba 16, 2024, yameratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Pamoja na hayo, Mkuu huyo wa Wilaya amewahimiza walimu wa michezo na makocha wa vilabu kutumia ujuzi waliopatiwa na wakufunzi katika mafunzo hayo kwa vitendo ili kuboresha kiwango cha michezo wilayani Ruangwa.
Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha sekta hiyo kwa maendeleo ya jamii.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa