Mkuu a wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, HASSAN NGOMA amewataka madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kuhakikisha wanaweka mkazo katika ukusanyaji mapato na kuacha kufanya mzaha kwakua malengo ya serikali yanapaswa kufikiwa kwa mujibu mipango iliojiwekea.
Ngoma ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani robo ya pili lililofanyika machi 1, 2023 wilayani humo ambapo mjadalawa mapato ulichukua nafasi kubwa kwa madiwani kulalamikia kuhusu uhaba wa mapato jambo linalochelewesha utekelezaji wa baadhi ya mambo yalio katika mpango wa maendeleo ya wilaya ya Ruangwa.
“Kasimamieni mapato, haitoshi kutoa kauli nzito nzito kwenye baraza halafu hakuna kilichofanyika,Ruangwa ni katika Halmashauri wabovu katika kukusanya mapato nje ya mapato ambayo yanakuja kupitia ufuta na korosho, kwahiyo tukasimamie mapato tuweze kuyafikia malengo ya kimaendeleo tulijiwekea na yalioagizwa na serikali” alisema Ngoma ambae ni mkuu wa wilaya ya Ruangwa.
Awali mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Frank Chonya alibainisha mpaka kufikia mwezi Februari mwaka huu Halmashauri imeshakusanya bilioni mbili milioni mia nane sabini na tano laki tatu kumi na mbili elfu n amia tano kumi na sita (2,875,312,516) sawa na asilimia 52% huku madiwani wakiwamo shabani kambona na Dareen Wolfram wakieleza kuwa wanataegemea Kwenda kufanya vikao na viongozi wa vijiji kuhamasisha na kushiriki katika kuhakikisha wanadhibiti shughuli za kuvuja kwa ukusanyaji mapato ili malengo waliyojiwekea yafikiwe katika kuleta maendeleo ya halamshauri.
“Hatujafikia hatua nzuri ya makusanyo kwa sababu tunacheza na vyanzo vya mapato vile vile vya zamani vyanzo vipya labda hivi vya vitalu vya madini kama tutapata mwekezaji, hata hivyo niytaenda kuanda mkakati na wakuu wa idara katani kwangu kuweka mipango kabambe ya kuthibiti mapato yanayotoroshwa katika kata ya nanganga” alisema kambona amabae ni diwani wa kata ya Nanganga wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa