Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mheshimiwa Hashim Mgandilwa amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri kumbadilishia majukumu ya kazi mtendaji wa kijiji cha mtimbo Ruangwa Chande .n.Chande.
Ametoa tamko hilo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha mtimbo kilichopo kata ya Likunja leo 06/12/2018.
Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo la kubadiishiwa majukumu mtendaji huyo kutokana na utoro kazini na kukwamisha maendeleo ya kijiji.
Amesema Mheshimiwa mtendaji Chande amekuwa na utaratibu wa kujichagulia muda na siku za kufika kazini na huku akijitapa kuwa yeye anajipangia apangiwi.
"Unakuwa muajiriwa wa serikali alafu unafanya mambo ya kijinga kama ya Chande wewe hufai kuwa muajiriwa wetu ukatafute kazi sehemu nyingine kabla sijakubaini siwezi kumfumbia macho mtu anaekwamisha serikali amesema Mgandilwa
Mkuu wa Wilaya amemtaka Afisa Utumishi wa Wilaya kutompangia kazi ya utendaji katika kijiji chochote kile kilichopo ndani ya Wilaya.
" Sitaki kumuona huyo katika vijiji vyangu mtoe umpeleke hata kufagia ofisini halmashauri na si katika hivi vijiji sitaki kumuona kabisa aiwezekani amrudishe nyuma Rais wetu" amesema Mgandilwa.
Naye bibi ngonza sidflide amesema mtendaji huyo amekuwa na tabia za kuwajibu kuwa yeye hawezi kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kwasababu yeye ni mwanachama wa Chama cha CUF.
Aliendelea amekuwa na tabia ya kutokufika kazini hivyo kusababisha wananchi kutokupata huduma wanazoitaji na akiulizwa anasema yeye anajipangia muda na siku ya kufika kazini.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa