Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe, Hashimu Mgandilwa amewataka viongozi wa vijiji kusimamia zoezi la upelekeaji maji na usombaji mchanga katika maeneo madarasa mapya yanajengwa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2021.
Amesema hayo tarehe 16/12/2020 alipofanya ukaguzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika shule ya Mnacho na Likunja.
Alisema Mhe, Mgandilwa wananchi wanapaswa kufanya kazi hizo mbili ikiwa ni mchango wao katika kuendeleza ujenzi katika maeneo yao.
“Kata zenye ujenzi wa shule za sekondari, Vijiji vina wajibu wa kushiriki kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa, na katika kutumia mfumo wa “force”akaunt wenye lengo la kupunguza gharama za ujenzi inapaswa kuchangia nguvu kazi kwa wakati kusaidia kwenye kupunguza gharama za maji na mchanga. Ambapo wanakijiji na wananchi wa maeneo hayo wanachangia nguvu kupunguza gharama. Aliwataka mafundi na wasimamizi wa madarasa wahakikishe yanakamilika kwa wakati”amesema Mgandilwa
Aliendelea kusema shule hizo ni kwa ajili ya watoto wetu hivyo kwa wazazi kupeleka vifaa hivyo ni sehemu ya wajibu wao katika kuhakikisha miundombinu ya shule za kata inakamilika kwa wakati.
“Sitaki mwezi wa kwanza wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapata shida ya madarasa. Hivyo wasimamizi hakikishenni ifikapo wakati wa kufungua shule majengo yawe yamekamilika kila kitu na kufaa kwa matumizi ya wanafunzi” amesema DC Mgandilwa
Aidha alisema haridhishwi na kasi ya ujenzi katika maeneo aliyotembele hivyo kuwataka mafundi waliopewa kazi waongeze mafundi ili kazi iende kwa kasi inayoitajika.
“Nitapita tena kufanya ukaguzi nataka nikute mafundi wameongezeka na kazi inaenda kwa kasi inayotakiwa ili mwezi wa kwanza wanafunzi wetu wasichelewa shule kwa ajili ya haya madarasa” amesema Mgandilwa
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa