Afisa Tarafa wa Mandawa Ndugu Msonga Matiku Magali kwa niaba ya Katibu Tawala Wilaya amewataka wanawake wajasiriamali wa Wilaya ya Ruangwa kutumia shughuli za maonesho zinazofanyika ndani ya Wilaya na hata Mkoa kama fursa ya kutangaza bidhaa zao ili kuongeza wigo wa masoko na kujikomboa kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Aprili 27, 2024 katika Kikao cha wanawake wajasiriamali wadogo wadogo (TWCC) wilayani Ruangwa kilichofanyika katika ukumbi wa Narungombe Pub.
Aidha, Ndugu Matiku ameendelea kuwasisitiza Wajasiriamali hao kuzalisha bidhaa bora zinazotangazika na kununulika katika maeneo tofauti tofauti ili kufikia malengo wanayoyatarajia.
" Mukiamua na kujipambanua mutafika mbali na yale mnayoyatamani muyafanye kwa vitendo yasiwe maneno tu ili kutimiza matarajio yenu" Amesema Matiku
Kwa upande wake, Afisa biashara Wilaya Ndugu Salim Mayala ametoa rai kwa wanawake wajasiriamali kujisajiri ili kutambulika na Serikali na kuweza kunufaika na mikopo ya asilimia 10.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa TWCC Mkoa Ndugu Pendo Joackim ametoa wito kwa wanawake wajasiriamali wa Ruangwa kutokata tamaa pindi wanapokutana na changamoto katika biashara zao halikadharika kuwa na ushirikiano miongoni mwao katika kuhakikisha mapambano yao katika biashara yanazaa matunda.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa