Mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi ambayo hulipia TShs 2000/= (Fomu Na TFN211) na kuambatanisha nyaraka zifuatazo:-
Kwa jina la biashara aweke nakala ya hati ya kuandikisha jina la biashara au kampuni kutoka BRELA.
Awe na uthibitisho wa uraia (Anaweza kuweka cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha mpiga kura, Taifa, pasi ya kusafiria au hati ya kiapo cha Mahakama).
Mwombaji awe na uthibitisho wa kuwa na mahali pa kufanyia biashara (nakala ya Hati ya nyumba au mkataba wa pango au stakabadhi ya malipo ya kodi ya majengo)
Mwombaji lazima awe na Hati/cheti cha utakaso wa Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA (Tax Clearance Certificate -TCC).
Kwa waombaji ambao sio raia wa Tanzania wawe na hati ya kuishi nchini ya daraja ‘A’ na kwa wawakilishi wa mfanyabishara au kampuni iliyoko nje ya nchi wawe na hati ya Kiwakili ( Power of Attorney).
Kwa biashara za kitaalamu awe na cheti cha utalaamu husika
Kwa biashara zinazodhibitiwa na Mamlaka za udhibiti awe na hati kutoka kwenye Mamlaka husika mfano TFDA, SUMATRA.
Kwa waombaji wanao huisha leseni zao watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita.
Baada ya ukaguzi na kujiridhisha matakwa yaliyotajwa, mwombaji husajiliwa kwenye mfumo wa usajili wa biashara wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa na kupatiwa namba za usajili na bill kwa ajili ya kulipia ada ya leseni husika kupitia benki ya NMB.
Ada za leseni ni kulingana na jedwali la viwango vya la mwaka 2014 ambapo utozwa kulingana na maeneo, aina ya biashara na kundi la biashara husika, pia ada hizo hulipiwa kila mwaka.