Wednesday 22nd, January 2025
@Viwanja vya Ngongo - Manispaa ya Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego wanawajulisha watanzania wote kuwa Maonesho ya Nanenane Kitaifa kwa mwaka 2017 yatafanyika Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo – Manispaa ya Lindi kama Mkoa ulivyopokea barua kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika yenye Kumb. Na. EA.18/45/01/121 ya tarehe 10 Februari, 2017.
Hivyo Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi, Wafanyabiashara na wadau mbalimbali mnaalikwa kuja kushiriki kwa kuanzia kipindi hiki cha maandalizi. Maonesho haya yanatoa fursa kubwa katika kuelezea shughuli mnazozifanya, kutoa elimu kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kuhusu mambo mbalimbali hasa katika uzalishaji bora, uongezaji thamani wa mazao, masoko na masuala mengine mengi.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu mtaarifiwa pale itakapokuwa tayari.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa