Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa, Mwl. George Mbesigwe, leo Agosti 25 amemkabidhi fomu ya uteuzi Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Ally Bakari Njalila, katika Ofisi za Uchaguzi za Jimbo la Ruangwa.
Njalila amefika katika ofisi hizo kwa ajili ya kuchukua fomu hiyo kama hatua ya kwanza ya safari yake ya kugombea Ubunge, na amebainisha kuwa ana dhamira ya kushirikiana na wananchi wa Ruangwa katika kupambana na changamoto zinazowakabili.
Amesema matarajio yake makubwa ni kuendeleza na kusimamia kwa vitendo mambo yote mazuri yaliyofanywa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo hilo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu unaendelea hadi Agosti 27, 2025, ambapo baada ya hapo uteuzi rasmi wa majina ya wagombea utafanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa