Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amekuwa mgeni rasmi katika sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani na kuwaagiza Maafisa utumishi kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira ya furaha na amani ili kuzifanya kazi zao kwa moyo wa kujitoa na mkunjufu.
Ameyasema hayo leo Mei 1, 2024 katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo Kimkoa yamefanyika Wilaya ya Ruangwa katika viwanja vya shule ya Msingi Likangara.
Mei Mosi ni siku iliyotengwa kwa heshima ya mchango wa Wafanyakazi katika sekta mbalimbali pia kuwawezesha kutambua haki zao.
Katika nchi nyingi, Maadhimisho haya ya siku ya wafanyakazi ni likizo Kitaifa ambapo hutoa fursa kwa Mashirika mbalimbali kuzindua kampeni maalum zinazoboresha na kujali maslahi ya wafanyakazi wao.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa