• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

IDARA YA MIPANGO NA URATIBU RUANGWA YAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA BAJETI WA IDARA/VITENGO

Posted on: September 26th, 2025

Idara ya Mipango na Uratibu ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa leo, Septemba 26, 2025, imeendesha mafunzo maalum kwa Maafisa Bajeti wa Idara/Vitengo kuhusu kuzingatia wakati wa uandaaji wa mipango na bajeti katika Halmashauri, ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yao.


Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, yakiwaleta pamoja Maafisa Bajeti kutoka Idara na Vitengo mbalimbali. Yamelenga kuwawezesha washiriki kuhakikisha kuwa maandalizi, usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango na bajeti unafanyika kwa kuzingatia taratibu, miongozo na viwango vya matumizi ya fedha za umma, huku yakiwasilishwa na Maafisa kutoka Idara ya Mipango na Uratibu, wakiongozwa na Pendo Njovu na Upendo Mkangara.


Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Uchumi, Pendo Njovu amesema:

“Mafunzo haya yatawapa ujuzi wa kina maafisa Bajeti katika Idara/Vitengo vyao, wataweza kuandaa mipango na bajeti kwa kuzingatia taratibu, miongozo na uwajibikaji” amesema Njovu.


Aidha, mafunzo yamewapa washiriki mwongozo wa kina kuhusu mbinu bora za kupanga bajeti kwa wakati unaofaa, kuzingatia vipaumbele vya Halmashauri na kuhakikisha kila Idara/kitengo kimeshirikishwa katika mchakato wa uandaaji wa bajeti. Lakini pia, wamejifunza namna ya kutengeneza mpangilio wa kazi unaowezesha kila hatua kufuatiliwa kwa wakati, na kuhakikisha mipango inatekelezwa kwa ufanisi.


Vilevile, washiriki wamepatiwa mafunzo ya vitendo kuhusu kuandaa mipango na bajeti kwa mujibu wa viwango vya kitaifa, pamoja na mbinu za kupima maendeleo ya utekelezaji wake. Mafunzo hayo yamehimiza pia umuhimu wa kuhakikisha kila hatua inafuatiliwa ili kuepuka ucheleweshaji wa miradi ya Halmashauri na kupunguza makosa ya kifedha.


Hata hivyo, Maafisa Bajeti wamejadili changamoto zinazojitokeza katika uandaaji wa bajeti na mipango, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa taarifa sahihi, upungufu wa mafunzo ya mara kwa mara na rasilimali chache za kiutendaji. Wamekubaliana kuwa mafunzo kama haya yamekuwa muhimu sana kuongeza uelewa na uwezo wa Maafisa Bajeti.


Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Bajeti wenzake, Afisa TEHAMA Wilson Dossa, ameshukuru Idara ya Mipango na Uratibu kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu, huku akiomba yafanyike mara kwa mara ili kuwaimarisha zaidi.“Mafunzo haya yamekuwa muhimu sana kwetu, na tunatumai yataendelea kufanyika mara kwa mara, ili tuzidi kuimarika” amesema Dossa.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA 27 MEI 2025 May 27, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • ZIMESALIA SIKU 16 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 13, 2025
  • ZIMESALIA SIKU 18 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 11, 2025
  • ZIMESALIA SIKU 23 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 06, 2025
  • ZIMESALIA SIKU 24 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

    October 05, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa