Saturday 21st, December 2024
@kiwanja cha CWT
Kuelekea siku ya maadhimisho ya wanawake duniani Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa anawakaribisha wanawake wote katika siku hiyo muhimu ya sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, itakayofanyika katika viwanja vya CWT mjini mkabala na kiwanja cha shule ya msingi Likangara.
Katika kusherehekea siku hiyo kutakuwa na Maandamano ambayo yataaanza yake katika eneo la kwa Mtota Saa 2:30 Asubuhi kuelekea kwenye viwanja CWT Ruangwa. Ratiba itaanza Saa 2:00 kamili asubuh na kumalizika Saa 7:20 mchana.
Mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Rashidi Nakumbya
Karibuni wote wanawake kwa wanaume mshike mkono jirani yako sote twende tukashereheke, ukiona tangazo hili mwambie na mwenzio.
*Kauli mbiu ya 2019 badili fikira kufikia ukawa wa kijinsi kwa maendeleo endelevu.*
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa