Wananchi wilayani Rungwa mkoani Lindi, watakiwa kutunza misitu ya asili ili iweze kuwaletea tija kiuchumia kupitia uvunaji wa kisasa unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Rai hiyo imetolewa tarehe 7 Octoba, 2022, na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Ruangwa Maisha Mtipa, alipokua anafungua kikao cha Tathimini ya uvunaji wa misitu wilayani humo iliofanyika katika ukumbi wa jengo la mkuu wa wilaya hiyo.
Akizungungumza katika kikao hicho Mtipa, ameshukuru shirika la kuhifadhi misitu Tanzania (TFCG) Kwa kutoa elimu juu ya matumizi bora ya Ardhi ikiwamo kuelimisha juu ya utaratibu wa utunzaji na uvunaji wa rasilimali misitu katika baadhi ya vijiji ikiwamo Kijiji cha Malolo ambapo wananchi wake wamepatiwa elimu hiyo iliyoanza kutekelezwa kwa vitendo na kuonyesha tija.
Aidha amesema ni muhimu sasa jamii ya watu wa Ruangwa kwa mfano wa Kijiji cha malolo kuhakikisha wanaendeleza utaratibu wa uvunaji bora wa rasilimali misitu ili ziweze kuwanufaisha kiuchumi na kuchochea maendeleo katika vijiji husika wilaya na Taifa kwa ujumla.
“taaluma hii ya uvunaji wa misitu kitaalamu tuhakikishe tunaitumia ipasavyo ili iweze kuleta mabadiliko katika vijii vyetu lakini hata kwetu mmoja mmoja kiuchumi kupitia mavuno tutakayoyafanya tutunze na tulinde uhifadhi wa misitu yetu ili iweze kuleta tija endelevu” Alisema Mtipa.
Athumani Rashidi ambae ni Afisa mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu ya mazao ya misitu alisema,mfumo wa uvunaji mkaa na Mbao endelevu unazingatia uendelevu wa ikolojia, rasilimali na motisha kwa jamii zinazosimamia misitu pamoja na kuzingatia hatua na masharti katika kutunza misitu na kubainisha kuwa kutotumia mbinu hizo kunasbabisha Taifa kupoteza mapato takribai bilioni 220 kwa mwaka zinzotokana na uvunaji wa mkaa.
Miongoni mwa walengwa walionufaika na mradi huo kutoka Kijiji cha malolo Frank Daudi mwambe, anazema tangu kuanza kwa mradi mwezi Agost 2021 mpaka sasa kupitia kikundi chao cha Likunga mkaa endelevu wamfanikiwa kuvuna gunia 120 mpaka sasa, ambapo amebainisha kuwa wameshapata soko ambalo kila gunia moja lenye ujazo wa kg 50 watauza kwa shilingi 8,000/=.
“Hatujaanza kuuza lakini tunategemea tukianza biashara hii itatusaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na serikali yetu ya Kijiji na tayari tumeshapata soko la kuuzia” alisema Daudi.
Alipoulizwa kuhusu namna wanavyoimarisha matumizi bora ya ardhi katika Kijiji cha malolo na namna ya kulinda misitu hiyo isivamiwe na wahalifu Andrea Gelion ambae ni moja ya wakata mkaa kijijini hapo alisema, wamekua wakifanya doria katika eneo la hifadhi ili kulinda misitu hiyo ikiwa ni Pamoja na kutoa hamasa kwa wana jamii kuzingatia uvunaji wa kisasa unaozingatia hatua za uvunaji endelevu.
Inaelezwa kuwa asilimia 96% nchini Tanzania jamii hutumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupika ambayo ni zaidi ya tani milioni 2.3 zinatumika kwa mwaka, hivyo matumizi ya uvunaji bora na endelevu wa rasilimali misitu Pamoja na kuongeza tija kiuchumia pia kutaimarisha utunzaji wa mazingira.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa