Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda amewapongeza wajasiliamali wa Ruangwa kwa kuleta bidhaa mbalimbali na kwa uwingi katika banda la Wilaya ya Ruangwa.
Amesema hayo leo tarehe 2/08/2019 wakati akitembelea katika banda hilo wakati wa maoneshe ya nane nane yanayofanyika kikanda ya kusini katika viwanja vya Ngongo.
Mheshimiwa Mmanda alisema wajasiliamali wamejitahidi kwenye kuleta bidhaa kwenye tamasha na amewataka Halmashauri husika kuwahamasisha wajasiliamali hao kushiriki tamasha la vijana litakalifanyika baada ya maenesho haya.
“Wamejitahidi kuleta bidhaa kuna tamasha la vijana baada ya maonesho haya ni fursa ya wao kuuza bidhaa zao wahamasisheni kwa wingi ili wapeleke bidhaa zao na wapate soko” amesema Mmanda
Sambamba na hayo Mkuu wa Wilaya alitoa pongezi kwa mfugaji wa n’gombe mwanamke Bi Sheri Nachinuku ambaye anafuga ng’ombe wa kisasa Wilayani Ruangwa.
Alisema yeye akawe mfano wa kuigwa na wanawake wengine ili na wao waanzw kujishughulishe na ufugaji kama huo kwani hiyo ni ajira inayoweza kurithishwa kutoka kwa mababu mpaka wajukuu.
Maoneshe hayo yameanza tarehe 1/ 08/2019 katika viwanja vya ngongo na yatafungwa rasmi tarehe 08/08/2019.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa