Mafunzo ya mfumo wa Gothomis Centralized yameendelea kwa wafawidhi wa vituo vya afya, departmental incharge wa Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, katibu wa afya, na maafisa wa TEHAMA, yakifanyika katika ukumbi wa hospitali hiyo leo Octoba 03, 2024, mafunzo hayo yanaendeshwa na mtaalam kutoka TAMISEMI kwa lengo la kuwajengea uwezo wafawidhi kuhusu usimamizi bora wa taarifa za afya.
Wafawidhi wa vituo vya afya wanajifunza jinsi ya kutumia mfumo wa Gothomis ili kuboresha utunzaji wa taarifa za wagonjwa na huduma za afya kwa ujumla. Mfumo huo unalenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa.
Mtaalam kutoka TAMISEMI ameweka wazi kuwa mfumo wa Gothomis utarahisisha ufuatiliaji wa taarifa za wagonjwa na kuongeza uwazi katika utoaji wa huduma. Pia, itawawezesha wafawidhi kusimamia kwa urahisi zaidi shughuli za kila siku za vituo vya afya na hospitali.
Mafunzo hayo yanaendelea kwa siku kadhaa, yakitarajiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa namna ya utunzaji wa taarifa na kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa Wilaya ya Ruangwa.
Ikumbukwe, GOTHOMIS Centralized (Government of Tanzania Health Operations Management Information System) ni mfumo wa kidijitali uliotengenezwa na Serikali ya Tanzania ili kuboresha usimamizi wa taarifa za huduma za afya katika vituo vya afya, zahanati, hospitali, na taasisi nyingine za afya. Mfumo huu unawezesha ukusanyaji, utunzaji, na ufuatiliaji wa taarifa za wagonjwa kwa njia ya kisasa, ikiwa ni pamoja na taarifa za matibabu, dawa, na huduma zingine zinazotolewa katika vituo vya afya.
GOTHOMIS Centralized pia unalenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa kurahisisha utunzaji wa takwimu, kutoa ripoti sahihi kwa wakati, na kusaidia maamuzi ya haraka na yenye tija kwa watendaji wa sekta ya afya. Mfumo huu unaunganisha vituo vya afya vilivyoko katika maeneo mbalimbali ili kuwezesha taarifa kutolewa na kufuatiliwa kutoka ngazi ya Wilaya hadi Kitaifa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa