Wakulima wanaolima zao la korosho wilayani Ruangwa mkoani Lindi, hususan wanaotokea katika vijiji vya Namikulo, chunyu na Liuguru, wamelalamikia kuwapo kwa vitendo vya wizi wa korosho zilizo mashambani kwa baadhi ya wananchi wasio waadilifu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti octoba 4, 2022, wanakijiji wakiwamo Mohamedi likonja wa Namikulo amesema kumekua na tabia za baadhi ya watu wasiofahamika kupita katika mashamba na kuokota korosho zilizopo kisha kuondoka nazo bila ya ridhaa ya mwenye shamba.
“Yaani sikuhizi ukichelewa tu Kwenda shambani kuokota korosho zilizoanguka tayari utashangaa unakuta zishaokotwa na alieokota hajulikani, kwahiyo ni wizi umezuka” Alisema Likonja.
Aidha kwa upande wake Bwana Mikidadi Ng’apuka ambae ni mkulima wa korosho Kijiji cha Chunyu amesema wizi uliopo pia mbali na kuokota korosho zilizoanguka pia kumekuwapo na tabia ya kupanda juu ya miti yenye korosho kisha kutikisa ili zianguke kwa wingi na zinapoanguka huzikusanya na kuondokana nazo pia.
“Wanaokota zilizondoka kwa upepo na kisha wanatikisa miti pia n ahata kupanda juu ili kutikisa zidondoke kisha wanaondoka nazo” alisema Ng’apuka
Walipoulizwa baadhi ya sababu zinazopelekea kutokea kwa hali hiyo Bwana Mahina ambae ni mkulima wa Kijiji cha liuguru ametaja sababu za kuwapo kwa hali hiyo ni kutokana na uuzaji holela uliozuka maarufu kama CHOMA CHOMA, na kutaja kuwa ndio sababu inayopelekea watu kuiba korosho ili wakauze kwa wanunuzi holela wanaopita mitaani.
“Sababu kubwa hap ani wanunuzi holela choma choa ndio maana mtu anaona bora aibe kisha auze kwakua hatajulikana lakini ingekua ghalani lazima wangejulikana maana kila mkulima kuna taarifa zake sasa mtu ambae si mkulim rahisi kumbaini” alisema.
Katika kuhakikisha suala hilo linadhibitiwa wakulima hao wameiomba serikali za vijiji kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi ili kuwadhibiti wezi hao Kwaku wakulima wanatumia ghalama kubwa kuandaa mashamba mpka kufikia hatua ya mavuno.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa