Vikundi 12 vya wanawake zaidi ya 140 wanaojihusisha na ufugaji wilayani Ruangwa Mkoani Lindi wamepatiwa msaada wa kuku kutoka wizara ya mifugo na uvuvi kwa lengo la kuwasaidia kuendelea kujikwamua kiuchumi.
Hatua hiyo inakuja kufuatia Ombi la Mbunge wa Ruangwa ambae ni waziri mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, kumuomba Naibu waziri wa Mifugo Abdallah Ulega, kupitia wizara yake kuwasaidia vifaranga vya kuku wafugaji hao wakati alipofika katika ziara yake ya kikazi wilayani humo.
Akikabidhi Vifaranga hivyo, mapema machi 16 mwaka huu, katibu wa mbunge wa Ruangwa Kasambe Hokororo amesema madhumuni ya kuku hao kwa wanavikundi ni kuwawezesha ili wajikwamue kiuchumi huku Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa George Mbesigwa akiwataka wanufaika kuwafuga kuku hao vizuri ili waweze kuzalisha kwa wingi.
Kwa mujibu wa Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Ruangwa Salum Msangi ni kwamba kuku hao waliwapokea kutoka wizarani wakiwa elfu tatu na wanakenda kuwagawa katika vikundi 12 ambapo kati ya hivyo vikundi 2 ni vya mashamba darasa watapa kuku 600 kila kikundi huku vikundi 10 ni vya wanachama vinavyotajwa kupata kuku 150 kwa kila kikundi.
Mwisho.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa