Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma akabidhi Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Milola kilichopo Manispaa ya Lindi leo Mei 29, 2024 ambao utapitia na kukagua miradi 8 ya maendeleo katika Manispaa hiyo.
Aidha Mhe. Ngoma awapongeza Viongozi, Wakuu wa idara na Watumishi wote kwa kushirikiana vyema katika shughuli zote za kuupokea Mwenge wa Uhuru mpaka kuukabidhi katika Manispaa ya Lindi.
Pia awashukuru vijana wa hamasa na wananchi wote kwa kujitoa kwao na kukubali kuacha familia zao ili kuhakikisha Mwenge wa Uhuru 2024 unapokelewa vizuri na kwa kishindo na unaagwa kwa shangwe lenye kuvutia.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa