Viongozi na Wataalam wa Wilaya ya Ruangwa wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Hassan Ngoma wamewasili wilayani Tanganyika Mkoa wa Katavi kwa lengo la kupata mafunzo kuhusu biashara ya hewa ukaa.
Mafunzo hayo kufanyika Machi 18, 2024 yakiongozwa na Afisa Misitu wa Wilaya ya Tanganyika Ndugu Ephraim Luhwago ambapo ametoa wito kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza misitu na maeneo yanayozunguka misitu.
" Inatakiwa kuwe na uwazi na kushirikisha wananchi ili wasiweze kuharibu misitu kwani biashara ya hewa ukaa ni biashara kubwa na ina faida kubwa ambayo huweza kukuza uchumi wa Halmashauri zetu" Amesema
Aidha, Luhwago ameendelea kusema kuwa biashara ya hewa ukaa ni biashara ya kimataifa na huwa inahusisha Halmashauri ya Wilaya, Mwekezaji na mnunuzi. Kwa upande wa mwekezaji ana faida ya 39% na Halmashauri ya Wilaya ina faida ya 61%
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Ngoma ametoa wito kwa viongozi na Wataalam wa Wilaya ya Ruangwa kuyatekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kuhusu biashara ya hewa ukaa katika Wilaya ya Ruangwa ili kuinua uchumi wa Halmashauri na kuwa wajumbe wazuri wa kutoa elimu kwa jamii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa Mheshimiwa Andrew Chikongwe ametoa shukrani kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kwa mapokezi mazuri na elimu ya kutosha tena yenye tija na kuahidi kwamba watatumia elimu hiyo kwa vitendo katika Wilaya ya Ruangwa ili kukuza uchumi wa Wilaya, Mkoa na Nchi kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa