Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wema wa Mama, Bi Wema Sepetu, ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, leo Machi 30, kupitia kampeni yake ya Wema wa Mama.
Ziara hiyo imelenga kujionea utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akiwa Ruangwa, Wema ametembelea miradi katika sekta ya afya, elimu, na maji, ambapo ameona ujenzi wa hospitali ya Wilaya yenye miundombinu bora na vifaa tiba, shule za msingi na sekondari, pamoja na maboresho ya miundombinu ya maji safi na salama kwa wananchi.
Aidha, Wema amepongeza juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania na amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo kwa maendeleo endelevu.
Kwa upande wao, wananchi wa Ruangwa wametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwaletea maendeleo.
Kwa kutambua juhudi za viongozi na Serikali, ziara hii imeimarisha ushirikiano kati ya jamii, wadau wa maendeleo na Serikali, jambo linalochochea utekelezaji endelevu wa miradi, ikichangia kuboresha huduma za afya, elimu na maji hivyo kuinua kiwango cha maisha ya wananchi kwa manufaa ya sasa na ya baadaye.
#RuangwakwaMaendeleoInawezekanaTimizaWajibuWako
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa