Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshuhudia makabidhiano ya matrekta kati ya Wizara ya Kilimo na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa katika hafla iliyofanyika leo, Februari 22, 2025, kwenye viwanja vya Stendi ya Nandagala.
Wilaya ya Ruangwa imepokea matrekta matano, ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kusambaza zana za kilimo kwenye vituo 45 vya utoaji huduma nchini. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Waziri Mkuu, ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa, Frank Chonya, amepokea matrekta hayo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omary.
Aidha, Mpango huo wa Serikali unalenga kuboresha sekta ya kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanapata nyenzo bora za kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa