Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea mabanda ya taasisi na wajasiriamali mbalimbali katika Kongamano la Wanawake linalofanyika katika viwanja vya Maegesho ya Malori leo, Machi 6, 2025.
Mabanda hayo yanatoa fursa kwa wanawake na wadau mbalimbali kuonesha bidhaa na huduma zao, kubadilishana uzoefu, pamoja na kujifunza mbinu bora za kuboresha uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao yao.
Kaulimbiu ya kongamano hilo kwa Kanda ya Kusini ni: “Ushiriki na Mchango wa Wanawake katika Kukuza Maadili, Uzalishaji na Kuongeza Mnyororo wa Thamani ya Mazao.”
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa