• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Waziri Mkuu azindua kiwanda cha kuchakata Muhogo

Posted on: March 22nd, 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara watumie fursa ya uwepo wa kiwanda cha kuchakata muhogo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi kwa kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kujiongezea kipato.

“Kama unataka pesa nenda kalime muhogo kwani kuna soko la uhakika na pia zao hili ni la muda mfupi na kilimo chake ni rahisi. Kwa sasa hatuna muda wa kukaa vijiweni vijana jiungeni katika makundi na muanzishe mashamba ya mihogo soko lipo tena mwenye kiwanda atawafuata hukohuko shambani bila kujali umbali wa eneo zao  lilipo.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo  Machi 22, 2019 wakati akifungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi.

Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli la kuhamasisha ujenzi wa viwanda ni kusaidia katika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini kabla ya kuuzwa.” Mbali na kuongeza tija kwa wakulima pia viwanda vinatoa ajira nyingi”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amekipongeza kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwa kazi nzuri ya utafiti wa mbegu za mazao mbalimbali wanayoifanya. Amesema kituo hicho ndicho kilichotafiti mbegu bora za muhogo zenye uwezo wa kuzalisha tani 20 hadi 50 kwa hekta.

Kwa upande wake, Balozi wa ufaransa nchini, Balozi Frederic Clavier amesema Serikali ya Ufaransa ipo tayari kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika mkakati wake wa kukuza uchumi hadi kufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.

Amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni ushuhuda tosha wa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kilimo ni miongoni mwa mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania.

Nae, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewashukuru wawekezaji hao kwa uamuzi wao wa kujenga kiwanda cha kuchakata muhogo nchini kwa kuwa wamewezesha wakulima wa zao hilo kupata soko la uhakika na vijana wengi kupata ajira.

Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msukumo alioutoa wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini kwa kuwa umechangia kuboresha maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

Mbunge huyo amesema uwekezaji katika sekta ya viwanda umesaidia kupunguza changamoto ya ajira hususani kwa vijana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa juhudi zake, kwani hatukutarajia kuwa na kiwanda katika eneo hili”.                                                                                                                                                                                                 Awali,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CSTC, Christophe Gallean alisema kiwanda hicho ambacho kilianza kujengwa mwaka 2012 kinazalisha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu cha ubora na kinauza unga huo katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani.

Alisema kiwanda hicho chenye wafanyakazi zaidi ya 420 ambapo Watanzania ni asilimia 97 kina uwezo wa kuchakata tani 60 za muhogo mbichi kwa siku, ambao ni sawa na tani 25 za unga bora wa muhogo kwa siku.

(Mwisho)

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa