• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

WAZIRI MKUU ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MRADI WA MAJI WA VIJIJI 55

Posted on: February 18th, 2023

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji utakaogharimu takribani shilingi bilioni 120 unaotekelezwa katika vijiji 55 vya wilaya za Ruangwa (vijiji 34) na Nachingwea (vijiji 21) mkoani Lindi.

Amesema mradi huo ambao utatekelezwa na wakandarasi wawili wazawa ambao ni STC Construction Company Limited na Emirate Builders Co. Limited unatarajiwa kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika wilaya hizo.

 

Waziri Mkuu ameshuhudia utiaji saini wa mkataba huo katika hafla iliyofanyika leo (Jumamosi, Februari 18,2023) kwenye ukumbi wa chuo cha VETA kilichopo Nandagala wilayani Ruangwa. Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakandarasi hao wakamilishe mradi huo kwa wakati.


 

Amesema katika kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi mingi ikiwemo ya maji ambayo ni  ahadi ya Rais ya kumtua mama ndoo kichwani.

 

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 ambayo inaielekeza Serikali kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini unafikia zaidi ya asilimia 85 na zaidi ya asilimia 95 kwa mijini ifikapo Mwaka 2025.

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi ametoa wito kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wahakikishe wanautekeleza kwa wakati na kwa uaminifu wa hali ya juu na kwamba wizara itawasimamia kwa ukaribu.

 

Naibu Waziri huyo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha dhamira yake ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani inatimia.

 

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Mhandisi Clement Kivegalo amesema upatikanaji wa maji Ruangwa kwa sasa ni asilimia 68.2 na Nachingwea ni asilimia 67, hivyo kukamilika kwa mradi huo ambao utanufaisha wakazi zaidi ya 130,000 kutawezesha watu wengi zaidi kufikiwa na huduma hiyo.

 

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack alitumia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia anazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo katika kipindi cha miaka miwili zaidi ya shilingi bilioni 300 zimepokelewa mkoani humo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ikiwemo ya elimu na afya.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa