• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Waziri Mkuu Ashiriki Ujenzi wa Uwanja Mpya

Posted on: May 25th, 2018

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki kazi za ujenzi wa uwanja mpya wa michezo wilayani Ruangwa kwa kubeba zege na matofali pamoja na wananchi.


Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, ameshiriki zoezi hilo leo kwenye uwanja huo unaojengwa katika kijiji cha Dodoma, kata ya Nachingwea, wilayani Ruangwa, Mkoani Lindi.


Akizungumza na wananchi na viongozi waliojitokeza kushiriki zoezi hilo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kazi ya ujenzi inayoendelea hadi sasa na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wana-Ruangwa kwa kurejesha moyo wa kufanya kazi kwa kujitolea


“Ninawashukuru sana wana-Ruangwa kwa sababu mmeanza kufanya kazi za kujitolea, haya matofali ni matokeo ya kazi yenu, hakuna hata mtu mmoja amelipwa kwa kazi hii. Nimeambiwa yanahitajika matofali 60,000 kwa ajili ya kujenga uzio lakini hadi sasa mmeshafyatua 57,000 na zaidi, ninawashukuru sana,” amesema.


“Nimeambiwa madiwani walipiga kambi ya wiki moja hapa, Umoja wa Vijana wa CCM nao walipiga kambi, UWT walikuja kusomba matofali, watumishi wa Halmashauri nao walipiga kambi, hongereni sana kwa kurejesha moyo wa kujitolea miongoni mwa wananchi,” amesema.


Katika zoezi la leo, walijitokeza wananchi wengi wakiwemo wazee, vijana na watoto. Baadhi ya watoto walikuwa wakibeba tofali moja kwa kushirikiana wawili wawili, watatu watatu hadi wanne.


Alisema ujenzi wa uwanja huo hadi sasa umeungwa mkono na wadau mbalimbali ambapo aliishukuru Benki ya CRDB ambayo imetoa sh. milioni 15 zilizotumika kununua mifuko ya saruji 1,200; Mbunge wa Kwimba, Bw. Mansoor Shanif Hiran mifuko 1,200 ya saruji; Mtibwa Sugar mifuko 2,000 ya saruji na TFF waliotoa mbegu za nyasi kwa ajili ya uwanja huo.


Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alipokea ahadi ya tani nne za nondo zenye thamani ya sh. milioni 10, kutoka kwa Kampuni ya Hyseas International Investment (T) Limited ya China.


Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa uwanja huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Afisa Utamaduni wa Wilaya hiyo, Bw. Simon Mwambe alisema awamu ya kwanza ya ujenzi inatarajiwa kukamilika Juni 2019 na hadi kukamilika kwake, uwanja huo utagharimu sh. bilioni 4.64.


Alisema uwanja huo ambao unajengwa kwa kutumia vipimo vya kimataifa, ukikamilika utawezesha watazamaji 10,500 kuingia uwanjani. Pia utajumuisha michezo mingine kama mpira wa miguu, pete, wavu, mikono, kikapu na riadha.


Naye Architecture Khalid Yassin ambaye alikuwa akitoa maelezo ya ujenzi wa uwanja huo kwa Waziri Mkuu, alisema utakapokamilika, uwanja huo utakuwa na kumbi mbili za kukutania wachezaji na makocha wao, vyumba vya kubadilishia, vyoo na ofisi ya meneja wa uwanja.

(Mwisho)
 



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa