WAZIRI MKUU KassimMajaliwa amesema hakuna kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwaumeme katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
Amesema Serikali imetengashilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyobado havijaunganishiwa nishati hiyo.
Waziri Mkuu alitoa kaulihiyo jana jioni (Jumanne, Julai 11, 2017) alipozungumza kwa nyakati tofauti nawananchi wa wilaya ya Ruangwa.
Waziri Mkuu ambayeameambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa aliyasema hayo katika mikutanoaliyoifanya kwenye vijiji vya Chiapi, Nandanga, Mbecha na Luchelegwa, ikiwa nisiku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.
“Rais wetu Dkt. JohnMagufuli anajali sana wananchi wake, hivyo ametenga fedha nyingizitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote vikiwemo na wilaya yaRuangwa. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”
Pia Waziri Mkuuamesema mwananchi hawatowajibika tena katika kulipia nguzo wala fomu zamaombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa naSerikali.
Waziri Mkuu aliongezakwamba lengo la Serikali ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzaniana kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola,jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa