WAZIRI MKUU KassimMajaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili wawezekujiajiri na kujikwamua kiuchumi.
Amekabidhi pikipiki hizo leo (Jumatano, Julai 12, 2017),baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingiLikangara.
Baada ya kukabidhipikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifukwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.
Amesema vijana wanaoendeshapikipiki maarufu bodaboda wanatakiwa kufuata sheria za usalama barabarani ilikuepusha ajali.
“Ukiendesha pikipikilazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wakona marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”
Wakizungumza baada yakukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendeshapikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametembeleamradi wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati ya Nandagala nakuridhishwa maendeleo yake.
Amesema kukamilika kwamajengo hayo kutarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma za afya kwa mama namtoto. Pia itawapunguzia kutembea umbali mrefu kwenda kufuata huduma hizokatika hospitali ya wilaya ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa