• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

WAZIRI MKUU AKABIDHI MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI RUANGWA.

Posted on: July 8th, 2022

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo Julai 08, 2022 amekabidhi mikopo yenye jumla ya shilingi, 256,158,000 iliyotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa vikundi 27 vyenye wanufaika 196.

Kati ya vikundi hivyo vya wanawake ni 14 ambavyo vimepewa mkopo wa shilingi 36,126,000. Vikundi vinane vya vijana vilipata mkopo wa shilingi 213,532,000 na vikundi vitato vya watu wenye ulemavu vilipata mkopo wa shilingi 6,500,000.

Akizungumza na wakazi wa kata ya Mandawa wilayani Ruangwa baada ya kukabidhi mikopo hiyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwa matumizi mazuri ya asilimia 10 ya makusanyo yao ya ndani ambayo yanatakiwa yatolewe mkopo kwa vikundi vya vijana (asilimia nne), wanawake (asilimia nne) na wenye ulemavu (asilimia mbili).

Waziri Mkuu amesema uamuzi wa halmashauri hiyo kutoa mkopo huo utaviwezesha vikundi hivyo kuongeza mitaji na uwezo wa kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali. “Vikundi vimewezeshwa kwa kuongezewa mitaji itakayoviwezesha kuzalisha kwa tija na kuweza kurejesha mikopo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wengine.”

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Frank Chonya amesema kati ya fedha hizo shilingi 214,658,000 zimetolewa kwa vikundi sita vya kimkakati ambapo kati yake vikundi vitatu vya vijana vinavyojishughulisha na usafirishaji wa abiria wa pikipiki vyenye wanufaika 20 vimepewa mkopo wa shilingi 57,132,000 zilizotumika kununua pikipiki 20.

“Kikundi kimoja cha vijana wa Kata ya Mandawa ambacho kina vijana 20 wanaojishughulisha na ufyatuaji wa tofali kimepewa mkopo wa shilingi 145,400,000 na kimenunua lori la tani nane litakalotumika kubebea mchanga na matofali. Pia kimenunua mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali yenye thamani ya shilingi 25,000,000 pia kimekopeshwa shilingi 10,000,000  kama mtaji.”

Amesema ili kurahisishia soko, Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa itakuwa inanunua matofali kutoka kwa vijana hao kwa ajili ya ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika wilaya hiyo. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya na elimu.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa vikundi vingine viwili vinavyojishughukisha na ufugaji kuku vyenye wanufaika 17 vilipewa mkopo wa shilingi 12,126,000 uliowawezesha kununua kuku 800 pamoja na vyakula vya kuku na dawa. “Pamoja na kutoa mikopo kwa vikundi vya kimkakati halmashauri imeendelea kutoa mikopo kwa vikundi vidogovidogo.”

Amesema mikopo yenye thamani ya shilingi 41,500,000 imetolewa kwa vikundi 20 vyenye wanufaika 133 ambapo kati yake vikundi vya vijana vine vyewe wanufaika 22, wanawake vikundi 12 vyenye wanufaika 95 na vikundi viwili vya watu wenye ulemavu vyenye wanufaika 16. “Kupitia utoaji huu wa mikopo jumla ya ajira 452 zimepatikana katika mwaka wa fedha 2020/2021 na mwaka 2021/2022 hivyo kupunguza uzululaji, uhalifu na utegemezi kwa vijana.”

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mandawa Issa Lipei ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.

  • MWISHO

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • MKURUGENZI WA RUANGWA AHIMIZA USAFI NA MAZOEZI KWA AJILI YA AFYA BORA

    May 10, 2025
  • SMAUJATA YAENDESHA ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WASICHANA RUANGWA

    May 09, 2025
  • BURIANI

    May 07, 2025
  • MHE. MAJALIWA AAINISHA MAFANIKIO MAKUBWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO RUANGWA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA

    May 03, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa