WAZIRI MKUU KassimMajaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhimagari mawili ya kubebea wagonjwa.
Amesema kati yamagari hayo moja ni kwa ajili ya hospitali hiyo ya wilaya na la pililitapelekwa katika kituo cha afya cha Mandawa.
Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo leo (Jumatano, Julai 12,2017), alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi.
Amesema magari hayo nimuendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afyakwa wananchi wake.
“Rais wetu Dkt. JohnMagufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabilizikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Waziri Mkuu amesema magarihayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa wagonjwa wanaohitajimatibabu ya dharura katika hospitali kubwa.
Kabla yakukabidhi magari hayo, Waziri Mkuu alitembelea wodi ya akina mamana ya watoto waliolazwa katika hospitali hiyo na amesema kwambaameridhishwa na hali ya utoaji huduma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, MheshimiwaRashid Nakumbya amesema magari hayo ni faraja kwao kwa kuwa walikuwa nachangamoto ya usafiri kwa wagonjwa wa dharura.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa