• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

WAZIRI KADUARA AZINDUA MAONESHO YA MADINI MKOA WA LINDI 2025

Posted on: June 11th, 2025

Maelfu ya wananchi na wadau wa sekta ya madini wamejitokeza kwa wingi leo Juni 11, 2025, katika Viwanja vya Madini vilivyopo Kilimahewa, wilayani Ruangwa kushuhudia uzinduzi rasmi wa Maonesho ya Madini Mkoa wa Lindi – (Lindi Mining Expo 2025.)


Mgeni rasmi katika uzinduzi huo amekuwa Mhe. Shaib Hassan Kaduara, Waziri wa Maji Nishati na Madini kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambaye amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa wadau wote katika kuchochea uchumi wa madini kupitia ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Aidha, katika hotuba yake Mhe. Kaduara amesema wananchi wanawajibu wa kulinda na kusimamia vizuri urithi wa madini yanayopatikana nchini. “Madini ni urithi wetu wa pamoja tukiyasimamia kwa umoja, yataleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya wananchi wetu.” Amesema Mhe. Kaduara


Maonesho hayo ya siku nne, yanatarajiwa kufikia tamati Juni 14, 2025, yamewakutanisha wachimbaji wakubwa na wadogo, wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, watafiti, taasisi za kifedha, wataalamu wa mazingira, pamoja na wananchi wanaotafuta fursa za kiuchumi kupitia sekta ya madini.

Kwa kuzingatia mwelekeo wa maonesho hayo, kauli mbiu ya mwaka huu ni: “Madini na Uwekezaji, Fursa ya Kiuchumi Lindi – Shiriki Uchaguzi Mkuu 2025”, ikisisitiza umuhimu wa rasilimali za madini katika kuchochea maendeleo ya Mkoa huku ikihamasisha ushiriki wa wananchi kwenye masuala ya kijamii na kidemokrasia.


Hata hivyo, maonesho haya yanatarajiwa kutoa jukwaa la kukuza uelewa, kuanzisha ushirikiano wa kibiashara na kuwezesha mnyororo wa thamani wa madini kufikiwa na wananchi wa kawaida – ikiwa ni sehemu ya ajenda pana ya Serikali za Mikoa na Serikali Kuu kuimarisha uchumi wa rasilimali.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA 17.11.2025 November 17, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA March 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI April 25, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III August 09, 2023
  • Ona zote

Habari mpya

  • HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA YAPATA USAJILI KWA MAFUNZO ENDELEVU YA KITAALUMA (CPD)

    November 20, 2025
  • MHE NGOMA AWAPONGEZA NMB KWA KUIPANDISHA THAMANI YA KOROSHO KWA WANANCHI WA RUANGWA

    November 18, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA LISHE KITAIFA 2025

    November 15, 2025
  • MAAFISA UTAMADUNI WAKUTANA NA WALAMBO, NGARIBA NA WAMILIKI WA VIWANJA VYA JANDO NA UNYAGO

    November 14, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa