Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Mb), ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mhe. Hassan Ngoma, pamoja na viongozi wa Chama na Serikali, katika ziara ya kukagua miundombinu ya Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kilichopo Wilaya ya Ruangwa, Septemba 20, 2024. Ziara hii ni sehemu ya mwendelezo wa Ziara Maalum Mkoani Lindi, inayolenga kufuatilia utekekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya awamu ya Sita.
Akiwa chuoni hapo, Mhe. Jafo ameeleza kuridhishwa na uendeshwaji wa mradi huo huku akisistiza umuhimu wa vyuo vya ufundi stadi katika kuandaa vijana wenye ujuzi stahiki kwa maendeleo ya taifa. Amewataka viongozi wa Wilaya kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha miundombinu hiyo inatumiwa kwa ufanisi.
Ziara hii imefanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone,” ikilenga kuonyesha matokeo chanya ya miradi ya Serikali inayoendelea kutekelezwa kwa manufaa ya wananchi wa Lindi na Taifa kwa ujumla.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa