Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Seleman Jafo, ameanza ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Ruangwa leo, Septemba 20, 2024, na kupokelewa kwa shangwe na wananchi wa Wilaya hiyo, ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unafanyika kwa ufanisi.
Ziara ya Dkt. Jafo imelenga kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Ruangwa, miradi hii ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita, ambayo inasisitiza utekelezaji wa miradi mikubwa ya kiuchumi na kijamii katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Kauli mbiu ya ziara hio ni, "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone," inaakisi dhamira ya Serikali ya Rais Samia kuhakikisha kuwa wananchi wanaona matunda ya juhudi zake za kuwaletea maendeleo, hii ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kufuatilia na kufaidi miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa.
Katika hotuba yake, Dkt. Jafo ameeleza kuwa Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaokubalika, amehimiza viongozi wa Wilaya kushirikiana kwa karibu na wananchi ili kuhakikisha changamoto zote zinazohusiana na utekelezaji wa miradi zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Katika hali ya sasa, Wilaya ya Ruangwa inaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa shule, barabara, miundombinu ya maji na huduma zingine za kijamii. Kwa kuangalia historia ya maendeleo ya Wilaya hii, tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika miaka ya hivi karibuni, huku matarajio ya baadae yakiwa ni kuifanya Ruangwa kuwa kitovu cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Ili kufikia lengo hilo, ushirikiano baina ya Serikali, wananchi, na wadau mbalimbali ni muhimu ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa