Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi amewataka wazazi na walezi mkoani lindi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa walimu wa kuzuia utoro kwa wanafunzi ili waweze kusoma na kuyafikia malengo yao.
Komba ameyasema hayo Disemba 12, 2022 katika viwanja vya CWT wilayani ruangwa mkoani Lindi alipomuwakilisha mkuu wa mkoa huo katika Maaadhimisho ya Siku ya Mwalimu wa Darasa la Kwanza yaliojikita kuhimiza na kusisitiza umuhimu wa walimu hao katika kusaidia kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi.
" wazazi nanwalezi shirikianeni na walimu hawa ili muweze kuwa na nguvu ya pamoja katika kutokomeza utoro ili kuwasaidia watoto wapate elimu kwa wakati stahiki" alisema komba.
Aidha katika hatua hiyo Mh. Komba ameahidi kuendelea kusimamamia maagizo ya serikali katika kuhakikisha huduma za chakula shuleni zinatekelezwa kwa kuwafikia wanafunzi ili wawe na hali nzuri ya kiafya itakayowasaidia kuwa na utayari mkubwa wa kuingiza maarifa.
Kwa upandewa baadhi ya walimu wa Darasala la kwanza waliojitokeza katika maadhimisho hayo wakiwamo mwalimu Emercia Fusi wa shule ya msingi msinjahili manispaa ya lindi na mwalimu Filemon Mponda wa Chimbila B wilaya Ruangwa, wamesema maadhimisho hayo yamekua yakiwasaidia kupata mbinu mpya za kufaragua zana mbali mbali za lufubdishia na kujifunzia na kubainisha kuwa huwasaidia pia katika kupata moyo zaidi na kuongeza bidii ya ufundishaji wa madarasa yao.
" maadhimisho haya yananisaidia sana kupata ubunifu mpya wa namna ya uundaji wa zana zaidi za kujifunzia kwa wanafunzi hivyo ni mazuri nayapenda sana" alisema Mwl. Mponda wa Chimbila B.
Awali akitoa tarifa kaimu afisa Elimu mkoa wa Lindi Mwalimu Hatibu Tuki, ameeleza mpango wa Mkoa huo kuwa ni kuhakikisha wanafunzi wote walioandikishwa wanaweza kusoma kuandika nankuhesabu.
Mkoa wa lindi ni miongoni mwa mikoa inayoengeza ufaulu wake kwa kasi katika matokeo ya darasa la nne, la saba, kidato cha pili kidato cha nne na kidato cha sita ambapo kwa mujibu wa taarifa ya matokeo ya darasa la saba mwaka 2022 mkoa umeongeza ufaulu kwa kufaulisha asilimia 93.07%.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa