Katika kuelekea kilele cha siku ya wanawake duniani, kamati ya sherehe hiyo katika Wilaya ya Ruangwa imetoa msaada kwa watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi Wilayani hapo
Msaada huo umetolewa leo tarehe 7/03/2020 katika hospitali ya wilaya na kukadhidhiwa kwa watoto hao na mwenyekiti wa kamati hiyo Diwani wa kata ya Ruangwa Mhe Alipa Mponda ambaye amekabidhi Juice, Madaftari, ndala, peni, maji, mabeseni na sabuni
Mhe alipa ametoa pongezi kwa watoto waliofika kupokea msaada huo kwa kujitambua na kutumia dawa kwa kufuata masharti ya wataalamu wanaowahudumia
Pia aliwataka wazazi na walezi kuwasimamia watoto hao katika matumizi ya dawa na lishe sahihi kwa watoto wanaotumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi.
Naye mratibu wa Ukimwi katika Wilaya Dokta Mariam Kimaro alisema watoto wengi ni yatima wanalelewa na walezi hivyo usimamizi wa matumizi ya dawa kwa baadhi ya watoto umekuwa wa kusuasua.
“ inaleta amani na faraja kuona watoto hawa wako vizuri kwenye masuala ya elimu na mambo ya kijamii *,* walezi wajitahidi kuwahimiza kumeza dawa kwani dawa hizo ndiyo msaada mkubwa kwao” Dokta Mariam
Vilevile Mwakilishi wa watoto wenye mahitaji maalumu alitoa shukurani kwa wazazi na walezi na manesi kwa kuwalea, kuwajali na kuwatunza bila kuwanyanyapa.
Mwakilishi huyo alisema wataendelea kujichunga na kutumia dawa na lishe bora kwa kufuata ushauri wa madaktari.
Wakati huo huo wanawake wa Ruangwa walifanya kongamano ya siku ya wanawake duniani jana
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa