• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

WATUMISHI LINDI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUJIFUNZA

Posted on: June 23rd, 2025

Watumishi wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kutumia ipasavyo fursa ya ushiriki wao katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Kitaifa kwa mwaka 2025 ili kujifunza na kuboresha utendaji wa kazi katika maeneo yao.


Wito huo umetolewa Juni 22, 2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bi. Zuwena Omary, alipotembelea viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma ambako maadhimisho hayo yanaendelea tangu Juni 16 na yanatarajiwa kufungwa rasmi Juni 23, 2025.


Akizungumza katika ziara hiyo, Bi. Zuwena amesema kuwa ushiriki katika maadhimisho hayo ni muhimu kwa sababu unawapa watumishi nafasi ya kuona na kujifunza mbinu bora kutoka taasisi na ofisi nyingine. Aidha, amesisitiza kuwa kujifunza kutoka kwa wengine ni njia mojawapo ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi serikalini.

Sambamba na hilo, Katibu Tawala huyo amewapongeza watumishi wa Mkoa wa Lindi kwa ubunifu waliouonesha katika mabanda yao na ushiriki wao hai katika kuwakilisha Mkoa kwa mafanikio.


Awali, Katibu Tawala Msaidizi (Utawala), Ndg. Nathalis Linuma, ametoa taarifa fupi kuhusu ushiriki wa Mkoa wa Lindi, akibainisha kuwa Halmashauri zote za Mkoa huo zimeonesha miradi bunifu katika utoaji wa huduma. Kwa mfano, Halmashauri ya Nachingwea imewasilisha huduma ya “One-Stop Centre”, Halmashauri ya Mtama imeonesha mfumo wa kidigitali wa utunzaji misitu na uvunaji wa hewa ukaa, huku Hospitali ya Mkoa ikiwa imewasilisha “Kadi_Alama”, mfumo unaosaidia kufuatilia utendaji kazi.


Mbali na hayo, Bi. Zuwena amepewa fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali kama TPDC, ambako ameangalia video ya utekelezaji wa mradi wa gesi asilia (LNG) unaotarajiwa kufanyika mkoani Lindi. Vilevile, ametembelea mabanda ya EWURA, LATRA, TFS, na Mbeya RS, ambako amepata elimu mbalimbali ikiwemo tiba asilia ya kudungwa na nyuki.

Kwa upande mwingine, watumishi wa Mkoa wa Lindi wametumia nafasi hiyo kumshukuru Katibu Tawala kwa kuwezesha ushiriki wao kwenye maadhimisho hayo na kwa kuandaa mazingira rafiki yaliyowawezesha kujifunza na kushirikiana kitaaluma na watumishi kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA 27 MEI 2025 May 27, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • WILAYA YA RUANGWA KUNUFAIKA NA MRADI WA URASIMISHAJI MAKAZI HOLELA

    June 24, 2025
  • WATUMISHI LINDI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUJIFUNZA

    June 23, 2025
  • DED RUANGWA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA RUANGWA VETERAN’S

    June 21, 2025
  • DC NGOMA AZINDUA UWANJA WA MICHEZO WA RUANGWA VETERANS SPORTS CLUB

    June 21, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa