Mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Hassan Ngoma amemuagiza mkuu wa polisi wilayani humo kufanya ukaguzi wa kampuni zote zinazojihusisha na ulinzi ili kuhakiki kama askari wanaowatumia awamepitia mafunzo ya kijeshi ikiwamo Jeshi la akiba.
Hatua hiyo inakuja kufuatia wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba 2022 wilayani humo kumueleza mkuu huyo kuwa miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni ukosefu wa ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
Hassan Ngoma akiwa katika zoezi la ufungaji wa mafunzo ya jeshi la akiba wilayani Ruangwa, licha ya uwapo wa changamoto ya ajira kwa vijana hao wa jeshi la akiba wanapohitimu amemuagiza mkuu wa jeshi la polisi wilayani humo kufanya ukaguzi wa makampuni ya ulinzi kujua sifa za askari wanaowatumi ikiwa ni Pamoja na kujua stahiki wanazolipwa kama zinaendana na kazi wanazofanya.
“Kuanzia jumatatu kufanyike ukaguzi kwa kampuni zote za ulinzi za wilaya ya ruangwa na taarifa hiyo iletwe ofisini kwangu, watu wote walioajiriwa ambao hawajapita katika jeshi la akiba waondolewe kwenye kampuni hizo mara moja” alisema Ngoma.
Miongoni mwa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba mwaka 2022 wilayani Ruangwa wakiwamo Pendo Namakonje, Sadat Nyagali na Yelusalem Kubila wamesema ni furaha kwao kuiona serikali inawajali kwa kuchukua hatua Madhubuti kuona namna wanavayowapa fursa vijana wanaohiyimu jeshi la akiba.
“Wengi wameajiriwa lakini hawajapitia mafunzo ya jesho la akiba kwahiyo endapo tutajiriwa sisi tuliohitimu mafunzo haya itasaidia kututtia moyo Zaidi vijana kuwa na uzalendo waw engine kuvutiwa kujiunga na mafunzo ya jeshi hili” alisema pendo Namakonje mmoja wa wahitimu mafunzo ya jeshi la akiba mwaka 2022 Ruangwa.
Wanafunzi walioanza mafunzo hayo wanatajwa kuwa 108 ambapo wanafunzi 18 walijiunga na jeshi la kujenga Taifa, 22 waliacha mafunzo kwa sababu mbali mbali na wanafunzi 68 ndio waliohitimu mafunzo hayo ya jeshi la akiba yaliendeshwa kwa muda wa wiki 16 sawa na miezi minne.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa