Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa utatekeleza zoezi la malipo ya ruzuku kwa kaya 3,889 zinazohusiana na Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kutoka Vijiji 90 vya Wilaya ya Ruangwa.
Zoezi hilo litaanza tarehe 18 Agosti 2025 na litakamilika Ijumaa tarehe 22 Agosti 2025. Aidha, kati ya Kaya hizo 3,889, Kaya 1,192 zitapokea malipo ya jumla ya Shilingi 44,532,000 kwa njia ya taslimu na kaya 2,697 zitapokea malipo ya jumla ya Shilingi 99,382,500 kwa njia za kielektroniki kupitia benki na simu.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa