Wanufaika wa mpango wa kaya masikini (TASAF) wameishuruku serikali ya awamu ya sita kwa kuwaletea elimu ya kuweka akiba na kukopa kupitia vikoba ambapo watacheza kwa sehemu ya hela wanazipokea kupitia mpango huo.
Wametoa shukurani hiyo wakati wa zoezi la upokeaji pesa lililofanyika katika vijiji vinavyonufaika na mpango huo wilayani Ruangwa.
Naye Katibu wa kikundi cha Litendaindu Ndg, Jafari Omari Machea wa mbekenyera alisema kupitia elimu waliyopewa ya vikoba wamejua na kuona faida ya kujiwekea fedha kupitia vikundi hivyo.
Aliendelea kusema wamejua fedha hizo ni akiba yao na watapata fursa ya kujikopesha kwa kufuata utaratibu walioelekezwa na watasimamia sheria zote ili vikundi vyao vya vikoba viwe endelevu.
Naye Fatma Ali Mnunduma wa Mmawa alisema wanashukuru waratibu wa zoezi la TASAF wilayani hapa kwani wanapata fedha zao zote kila zoezi la uhawilishaji linapofika.
Pia alisema zoezi la uhawilishaji fedha kwa njia ya bank litarahisisha na kupunguza msongamano katika ofisi za vijiji siku ya kupokea fedha hizo, hivyo aliuomba uongozi kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu ili watu wajiunge na mfumo wa bank.
Naye Bi Fatma abdala hasani alisema kuwa kupitia TASAF familia yake inapata matibabu kupitia mfumo wa CHF iliyoboreshwa hivyo utaratibu wa kulipia bima ni mzuri na unawasaidia.
Alisema wanufaika wengine wanaweza kuona bima haina umuhimu ila ukiugua na ukapata huduma ndiyo utajua umuhimu wa bima TASAf sasa hivi inatusaidia katika mambo muhimu zaidi.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa