Wanawake na wasichana wa Wilaya ya Ruangwa wamejitokeza kwa wingi leo, Machi 5, 2025, katika kilele cha Siku ya Wanawake kiwilaya, ambapo wamefanya maandamano ya kihistoria katika viwanja vya Shule ya Msingi Likangara, maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu ya mwaka huu, “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji,” ikilenga kuhamasisha jamii kuhusu haki za wanawake, usawa wa kijinsia, na mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo ni Kaimu Mtendaji wa FEMATA (Federation of Miners’ Associations of Tanzania), Bi. Kuruthum Runje, ambaye ataongoza hafla hiyo akiwaongoza wanawake na wadau wa maendeleo kuunga mkono juhudi za kuwezesha wanawake katika sekta mbalimbali.
Aidha, Katika miaka ya nyuma, ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi ulikuwa mdogo, lakini kupitia juhudi za Serikali na wadau wa maendeleo, hali hiyo imeanza kubadilika. Hata hivyo, bado kuna changamoto kama vile ukosefu wa fursa sawa katika sekta ya uchumi na elimu, Ili kufanikisha maendeleo endelevu, jamii inapaswa kuendelea kuhamasisha elimu kwa wasichana, kuwawezesha kiuchumi, na kuhakikisha usawa wa fursa kwa wote.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa