Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imefungua rasmi ghala la kuhifadhia mazao ya biashara lililopo kata ya Ruangwa katika kijiji cha lipande
Ghala hili lenye thamani ya shilingi Bilioni 6.6 fedha iliyotoka Serikali kuu kwa ajili ya uendeshaji wa miradi ya mkakati limeanza kutumika leo tarehe 12/11/2019.
Wakati wa uingizaji wa korosho katika ghala hili Mkuu wa Wilaya Hashim Mgandilwa aliwataka viongozi wa Ushirika kuhakikisha wakulima wanachambua korosho zao kabla ya kufika katika ghala
Mhe. Mgandwila ametoa kauli hiyo kutokana na kugundulika kuwepo na korosho ndogondogo zisizo na ubora zinazopelekwa ghalani.
“Ghala letu ndiyo linaanza tusijiharibie kwa kupata sifa mbaya ya kuwa korosho zisizo na ubora kuhakikisha hili inatakiwa tujikague wenyewe mapema kabla korosho hazijafika katika vyama vya ushirika” alisema Mgandilwa
Aidha Mhe Mgandilwa aliwataka wakulima kupanda miche ya mikorosho mipya ili kuepukana na kupata korosho ndogo ambazo zinapatikana kutoka katika miti ya zamani.
“Hili jambo linawezekana kuwa historia Ruangwa kinachotakiwa wakulima kupanda miche mipya kwa wingi ili kupata korosho zilizobora na hili linawezekana wanaruangwa msiniangushe” alisema Mgandwila
Vile vile amewataka vijana wanaotaka kubeba magunia ya korosho katika ghala kujisajili kwa kufuata matakwa ya kisheria ili waweze kupata kazi hizo
“vijana wa Ruangwa huu ni wakati wenu wa kupata ajira hapa ghalani waoneni watu wa ushirika wawasaidie nini mfanye ili msajiliwe kama ushirika maalumu cha kubeba mizigo” Mgandilwa
Ghala moja lenye uwezo wa kubeba tani 10000 kati ya mawili yaliyojengwa limeanza kufanya kazi kwa kuhifadhia korosho na ujenzi unaendelea katika hatua za ukamilishaji wa majengo yote na Korosho zilizopo katika ghala hilo zinatapigwa mnada siku ya jumapili Novemba 17/2019 Ofisi ya Ruangwa AMCOS.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa