Waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki mbili Kwa wataalamu wa Mamlaka ya maji Wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Ruwasa, kuhakikisha wakazi wa kata ya Nandagala pamoja na Taasisi tatu shule ya sekondari marry Majaliwa,chuo cha veta pamoja na zahanati zinafikiwa na huduma ya maji.
Waziri Aweso ameyasema hayo September 18, 2022 alipokua katika ziara yake ya kikazi kata ya nandagala wilayani ruangwa mkoani Lindi."Tumetoa milioni 100 wataalam hakikisheni wananchi na taasisi zinapata maji ili kuendelea na mahitaji muhimu ya wananchi"
Awali Diwani wa kata ya Nandagala ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Andrew Chikongwe amesema taasisi tatu zote zimekamilika lakini wanafunzi veta wanashindwa kupokelewa Kwa ukosefu wa maji huku akisema adha imekua kubwa Kwa wananchi ikiwa msimu wa kiangazi wananchi wananunua maji Kwa bei kubwa.
Hata hivyo mkurugenzi wa bonde la Ruvuma Jumanne Sudi Mpemba amesema wamefanya tafiti katika mabonde hivyo maji yatawafikia wananchi Kwa wakati huku Mhandisi wa maji mamalaka ya making wilaya ya Ruangwa, Laurence Mapunda akieleza kutegemea chanzo cha mradi wa maji chemchem iliyopo kijiji cha nga'u kwani wakati wa usanifu wa chanzo hicho cha maji kilikua na uwezo wa wa kutoa maji Mita za ujazo 7 Kwa Saa.
Mapunda ameongeza kuwa Changamoto kubwa ni kupungua Kwa uwezo wa chanzo hicho cha maji hasa kipindi cha kiangazi hivyo kupelekea adha kubwa ya maji ameongeza Kwa kumuahidi waziri kufanya Kazi ili wananchi waondokane na adha ya maji.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa