Wakulima wa korosho wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale, mkoani Lindi wanaohudumiwa na chama kikuu cha RUNALI wamekubali kuuza korosho zao katika mnada uliofanyika katika ghala la Lipande wilayani Ruangwa mkoani humo Oktoba 30,2022 kwa bei juu ya shilingi 1,855/= na bei ya chini shilingi 1,810/= kwa kilo moja.
Licha ya kuwapo kwa migomo ya wakulima kutoka katika baadhi ya vyama vilivoanza katika uuzaji wa zao la korosho msimu wa mwaka 2022/23, kwa kueleleza kuwa bei ya ununuzi ni ndogo katika mikoa ya Lindi na Mtwara wakulima wanaohudumiwa na chama kikuu RUNALI kwao imekua tofauti katika mnada wao wa kwanza wameridhia kuuza korosho zao na kubainisha kuwa wanauhitaji wa pesa ili ifanye maendeleo waliojipangia.
Wakizungumza baada yam nada huo mmoja ya wakulima wa zao hilo wilayani Ruangwa Mwanaidi Chimbunga alisemawamridhika na bei kutoka na kukaa kwa muda mrefu na ukali Maisha hivyo kuuzwa kwa mazao yao kutasaidia kupunguza changamoto zinazowakabili kutokana na ukata wa fedha.
“Mimi nimeridhika na hizi bei kwa sababu tumekaa muda mrefu na ukali wa Maisha, mimi kama mama nina Watoto wanasoma nilishindwa kuwapeleka shuleni kwahiyo kama imetokea hii fursa ya mnunuzi kununua zao langu binafsi nashukuru sana,” alisema Mwanaidi
Awali mkurugenzi mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred aliwaeleza wakulima sababu zinazopelekea kushuka kwa bei ya zao la korosho msimu huu kwa kubainisha kuwa sababu kuu ni wanunuzi wakuu kuwa na kiasi kikubwa cha korosho za mwaka uliopita, huku mwenyekiti wa chama kikuu RUNALI, Odas Mpunga akibainisha Zaidi madhara ya korosho hizo kama zinageendelea kubaki katika maghala kuwa zitazidi kunyauka na kupungua ubora hivyo wakulima wanaweza kupata hasara Zaidi kama wasingeridhia kuziuza kwa wakati.
“Korosho zinapoendelea kukaa ghalani zinanyauka na hivyo zinapungua uzito n ahata ubora wake kwahiyo kama wakulima watakua na migomo ya kuuza ni hasara kwao n ahata kwa vyama vya ushirika kwa maana zao litazidi kukosa soko kwa kupungua Zaidi ubora kutokana na kukaa” alisema Mpunga mabae ni Mwenyekiti wa chama kikuu RUNALI.
Jumla ya tani 6,000 zimenunuliwa kutoka wilaya za Liwale Ruangwa na Nachingwea ambapo wakulima waliowasilisha mazao yao ghalani watalipwa stahiki zao ndani ya siku kumi baada ya mnada huo kufanyika.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa