Wakulima Wilayani Ruangwa walalamikia vifungashio vya bidhaa zao vinavyoletwa na wafanyabiashara wanaokuja kununua mazao Wilayani humo.
Wamesema vifungashio hivyo vimekuwa vinawanyonya wao kwa kiasi kikubwa kwani vinakuwa vikubwa hali inayopelekea kuwekewa bidhaa nyingi kuliko fedha wanaopokea.
Mdahalo huo ulifanyika tarehe 26/06/2019 katika ukumbi wa Rutesco Ruangwa mjini ulijumuisha wakulima, wafungaji na wanunuzi wa mazao kutoka maeneo mbali mbali ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali Aghakani foundation.
Sambambamba na hayo Wafanyabiashara nao wamelalamikia kukosekana kwa masoko maalumu Wilayani humo hali inayopelekea kutokea kwa mifumuko ya bei ya bidhaa kwenye baadhi ya maeneo.
Waliuomba uongozi wa Halmashauri kuweka masoko maalumu ya kununulia bidhaa zao Ili kuwe na usawa wa bei ya manunuzi ya bidhaa kwa Wilaya nzima.
Aidha waliushukuru uongozi wa Aghakani kwa kuwakutanisha wadau hao wameweza kuzungumza changamoto za kibiashara wanazokutana nazo na watajitahidi kurekebisha yale yaliyobainika ni kikwazo panda zote.
Naye Afisa Mradi Kilimo biashara Wilaya ya Ruangwa kutoka shirika la Aghakani ndg, Jafari Sheshui alisema lengo la shirika la Aghakani kufanya mdahalo huo ni kuwasaidia wakulima wa Ruangwa kupata masoko na kujua wanunuzi wanaitaji bidhaa za aina gani katika masoko hayo.
Amesema Shirika lina lengo la kumsaidia mkulima kuona anafaidika na zao lake na kujua nini kwenye masoko wananunuzi wanaitaji na ndiyo maana limetoa nafasi ya kuwakutanisha wadau hawa muhimu wanaoitajiana.
Mwisho
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa