Wananchi wa Kijiji cha Nanjaru kilichopo kata ya Nambilanje wilayani Ruangwa Mkoani lindi, wameiomba Serikali kusaidia kuongeza ukubwa wa kituo kwa kuongeza majengo na wahudumu kutokana na Zahanati hiyo kuelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa inayotokana na kuwapo na idadai kubwa ya wageni walioingia siku za hivi karibuni ambao ni jamii ya wafugaji na wakulima.
Wananchi hao waliendelea Kusema kutokana na ongezeko la wakazi kijijini hapo wanaomba wajengewe kituo cha afya ili wapate huduma nyingi za afya.
Wakizungumza katika mkutano wa adhara uliofanyika tarehe 16/05/2022 kijijini hapo mbele ya mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma, wananchi hao wameomba kuongezewa wahudumu wa Afya ambapo kwa sasa wana wahudumu wawili pekee na kueleza kuwa jamii ya watu wa Nanjaru huzaliana sana jambo linalopelekea zahanati hiyo kuelemewa kwa idadi kubwa ya wagonjwa.
Aidha akijibu baadhi ya hoja Muuguzi mkuu wa Halmashauri ya wilaya Ruangwa Dkt. Adidas Iswalala, amesema anatambua changamoto zinazoikabili zahanati na wakazi wa kijiji hicho na kwamba ajira mpya zilizotangazwa na serikali zitatua changamoto hizo kwa kutoa kipaumbele kuwaongezea mtaalam wa Afya atakaesaidia katika kutoa huduma kijijini hapo.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa