• Anuani zetu |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Ruangwa District Council
Ruangwa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Uongozi wa Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Usafi na Mazingira
      • Kata
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Tehama
    • Kata
      • Nandagala
      • Mbekenyera
      • Likunja
      • Mnacho
        • Nangumbu
      • Malolo
      • Nachingwea
      • Ruangwa
      • Makanjiro
      • Mbwemkuru
      • Narungombe
      • Nangumbu
      • Luchelegwa
      • Chinongwa
      • Mandawa
      • Chunyu
      • Matambarale
      • Nkowe
      • Nambilanje
      • Nanganga
      • Namichiga
      • Mandarawe
      • Chibula
      • Chienjele
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Mradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi ya Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Videos
    • Hutuba
    • Albamu ya Picha
    • Habari
    • Tukio
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Wakandarasi acheni kulipua kazi zingatieni viwango-Majaliwa

Posted on: March 16th, 2019


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakandarasi wanaojenga majengo mbalimbali nchini yakiwemo na ya Serikali wahakikishe wanazingatia viwango na waache kulipua kazi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wakandarasi wawafundishe kazi mafundi wasaidizi wanaowatumia katika ujenzi wa miradi malimbali ili waweze kunufaika kwa kuongeza ujuzi.

Ametoa wito huo  leo mchana (Jumamosi, Machi 16, 2019), alipotembelea miradi mbalimbali ya ujenzi wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ukiwemo wa Hospitali ya wilaya.

Amesema Serikali inatoa pesa kulingana na kazi inayotakiwa kufanyika, hivyo amewataka wakandarasi wafanyekazi wanazopewa kwa kufauata taratibu za kiufundi na si ‘kulipua lipua’.

Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakandarasi hao kuwatumia mafundi wasaidizi waliopo kwenye maeneo ya karibu na miradi husika ili nao waweze kupata ajira.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka mafundi wasaidizi wahakikishe wanafanyakazi kwa bidii na uadilifu ili wawe mabalozi wazuri, jambo litalalowawezesha wengine kupata kazi.

"Nataka niwaambie mkifanya kazi kwa uaminifu wakandarasi watawachukua na kuwapeleka katika maeneo mengine wanayopata mradi. Jitumeni acheni uvivu mtafika mbali.

Amesema Serikali inatengeneza ajira kwa vijana kupitia wakandarasi wanaotekeleza miradi, hivyo wakandarasi wanatakiwa wawatumie mafundi wasaidizi walioko kwenye maeneo ya miradi.

Waziri Mkuu amesema amefarijika sana kuona vijana wanapata ajira na amewataka  watumie nafasi hizo kujifunza ufundi ili nao waje kuwa mafundi wakubwa na kuajiri wenzao.

Naye,  fundi msaidizi wa jengo la utawala katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa,Hamisi Ali amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwapelekea miradi mkubwa ambayo inawapatia ajira.

Ali ametoa wito kwa vijana wengine waache kukaa mitaani na badala yake wajitokeze na wachangamkie fursa za ajira zilizopo kwenye maeneo yao na wafanye kazi hizo kwa bidii.

Waziri Mkuu ametembelea ujenzi wa hospitali ya wilaya, ghala, Ujenzi wa ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Shule ya Seondari ya  Wasichana Lucas Maria.

 (mwisho)





Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA November 08, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA WAHUDUMU WA AFYA 872 KWA NGAZI YA JAMII HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA July 09, 2024
  • TANGAZO LA AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA August 01, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA 27 MEI 2025 May 27, 2025
  • Ona zote

Habari mpya

  • ZIMA MOTO WAENDESHA MAFUNZO YA TAHADHARI YA MAJANGA KWA WATUMISHI RUANGWA

    July 15, 2025
  • MAAFISA MIFUGO RUANGWA WAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO

    July 11, 2025
  • MAAFISA MIFUGO RUANGWA WAPATIWA MAFUNZO KUELEKEA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO

    July 11, 2025
  • PONGEZI

    July 11, 2025
  • Ona zote

Video

MAENDELEO YATAKUJA KWA KULIPA USHURU, TOZO NA ADA ZA HALMASHAURI. MWANANCHI LI0A KODI KWA MAENDELEO YETU
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Mpango wa Bajeti 2017/2018(MTEF)
  • Watumishi Portal

Kurasa zinazofanana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • BARAZA LA MITIHANI

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani zetu

    Ruangwa

    Anuani ya Posta: S.L.P 51

    Simu ya Mkononi: 0732932312

    simu: 0732932312

    Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa