Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe, Mashimba Mashauri Ndaki amewataka wafugaji kufuata sheria, kanuni na taratibu za maeneo ambayo wanaishi na kuacha ubabe .
Amesema hayo wakati wa kikao cha wadau wa mifugo na wakulima kilichofanyika tarehe 22/12/2020 Wilaya ya Liwale.
Katika kikao hicho kilichohuzuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, aliyewaongoza wakuu wa wilaya, wakurugenzi pamoja ,maafisa wa serikali na wadau wa kilimo na mifugo wa Mkoa wa Lindi waziri Ndaki amesema zipo taarifa kwamba wafugaji wanalalamikiwa kwa kuwatisha wakulima na kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima.
“Kila mtu ana haki ya kuishi popote ila huwezi kuishi kwa kutishia watu amani, wafugaji wengi ni wageni Katika Mkoa wa Lindi mnapaswa kuishi kwa kufuata taratibu na kuacha maisha ya ubabe ubabe” amesema Waziri.
Pia amewataka watendaji wa Kata, vijiji na viongozi wa Serikali za vijiji kuacha urafiki wa kinafiki wanaofanya na wafugaji kwani wao ni viongozi hivyo hawapaswi kufanya urafiki wa aina hiyo.
“Huo urafiki wenu unaumiza wanakijiji wengine acheni mara moja na ukibaikinika kiongozi unafanya hayo utachukuliwa hatua za kisheria” amesema ndaki
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe, Godfrey Zambi amewasisitiza wafugaji kuacha kutoa rushwa kuwataka wafuate sheria zinavyotaka
Aliendelea kusema kuwa wafugaji wamekuwa wakitoa fedha kwa watu wanaotaka wawasaidie kupitisha mifugo bila kufuata taratibu wakidhulumiwa wanaanza kulalamika.
Ameeleza kuwa hali hiyo hujitokeza kwa sababu wafugaji wamekuwa wanataka njia za mkato zisizo na uhalali na kuwahimiza wafuate taratibu zinavyotaka.
Aidha aliwataka wafugaji kupunguza mifugo kwa kuwauza na kupata kipato cha kuwaboreshea maisha yao au kuwekeza katika vitega uchumi vingine.
“Wafugaji wengi mnaishi katika mazingira ambayo hayaridhisha uzeni mifugo yenu mjenge nyumba nzuri na boresheni maisha yenu mifugo hiyo ni utajiri kwenu” amesema Zambi.
MWISHO
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa