Kuelekea maadhimisho ya kilele cha Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika kesho Aprili 26, viongozi na wananchi wa Wilaya ya Ruangwa wameadhimisha kwa kupanda miti katika Shule ya Msingi Dodoma, iliyopo Kata ya Nachingwea.
Zoezi hilo limefanyika leo Aprili 25, likiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Mhandisi Zuhura Rashid, ambaye ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki Bonanza la michezo litakalofanyika katika uwanja wa shule hiyo kesho, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Muungano.
Aidha, kupanda miti kumelenga kuboresha mazingira ya shule hiyo na kuchangia juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya ya Ruangwa.
Kwa upande mwingine, Maadhimisho hayo ni sehemu ya kumbukumbu muhimu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu inasema:
“Muungano Wetu ni Dhamana, Heshima na Tunu ya Taifa, Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.”
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa