Viongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakiongozwa na Katibu Tawala Wilaya Mhandisi Zuhura Rashidi watembelea kitengo cha matibabu ya watoto njiti na kutoa msaada kwa watoto hao pamoja na kujifunza jinsi ya kuwatunza na kuwalea watoto hao.
Kitengo cha matibabu ya watoto njiti katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwa kipo katika Hospitali ya Wilaya pekee ambacho hujikita kuwasaidia ambao wanashindwa kupumua wenyewe na kuhitaji msaada ya mashine ya kupumua na mashine ya joto halikadhalika husaidia watoto wenye manjano na kuwasaidia wale watoto wanaozaliwa na homa kali.
Wakizungumza na Viongozi wa Wilaya ya Ruangwa, Wauguzi katika Kitengo cha Matibabu ya watoto njiti Ndugu Shifra Mongo na Daudi George wameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kusogeza karibu kitengo hicho na kuwasaidia kuokoa maisha ya watoto wengi wanaozaliwa chini ya miezi 9.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa