Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo huadhimishwa Aprili 26 kila mwaka, Viongozi wa Wilaya ya Ruangwa wakiongozwa na Katibu Tawala Wilaya Mhandisi Zuhura Rashidi watembelea shule ya msingi Namakonde leo April 19, 2024 na kuongoza zoezi la kufanya usafi ambalo limehusisha Viongozi na wananchi mbalimbali na kutoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Wakati anakabidhi msaada huo Mhandisi Zuhura Rashidi ametoa shukrani kwa Viongozi wote wa Serikali kuu, Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Taasisi zote ambazo zimeshiriki katika zoezi hilo, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kukubali kuacha majukumu yao na kuungana na viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kufanikisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Ndugu Frank Fabian Chonya ametoa wito kwa wananchi kuendeleza umoja na mshikamano katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kutela maendeleo Chanya katika Wilaya.
Katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Ruangwa Mhe. Alipa Mponda kwa niaba ya Diwani wa Kata ya Nachingwea amewashukuru Viongozi na wananchi wote ambao wamejitoa kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu katika shule ya Msingi Namakonde na kuwaomba moyo huo wa kutoa uwe endelevu kwa wale wote wenye uhitaji katika wilaya ya Ruangwa.
Ruangwa
Anuani ya Posta: S.L.P 51
Simu ya Mkononi: 0732932312
simu: 0732932312
Barua pepe: ded@ruangwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa